Huduma za Meno
Huduma za meno zinazokua pamoja nawe na familia yako katika kliniki kote Missouri. Pia tunakubali Medicaid.
Chris Heinzel alihitimu kutoka Illinois Central College na kupata diploma ya Usafi wa Meno. Baada ya kuhitimu, Chris alijiunga na Jeshi la Wanamaji la Marekani ambako alihudumu kama msimamizi msaidizi wa huduma za usafi wa meno. Amekuwa akitoa huduma bora katika Jordan Valley Health tangu 2022.
Alipokuwa akihudumu katika Jeshi la Wanamaji, Chris alishauriwa kufikiria kujiunga na Shule ya Mafunzo ya Ufundi wa Meno. Mwanzoni alivutiwa na programu hiyo kwa sababu ilikuwa jambo ambalo angeweza kufanya ili kuwasaidia watu. Chris anafurahia jinsi taaluma yake inavyomwezesha kuwasaidia watu huku akijenga mahusiano ya kudumu. Anapenda kuona wagonjwa wakifurahi wanapoboresha afya yao ya kinywa. Chris pia anafurahia kuweza kuwasaidia watu wanapokuwa na wasiwasi. Anafanya hivyo kwa kuwatuliza na kuwahakikishia kwamba watatunzwa vizuri na watafurahi watakapomaliza matibabu yao. Kwa kufanya hivyo, Chris anatumaini si tu kuwasaidia wagonjwa wake, bali pia kuwaelimisha kuhusu matatizo yao ya sasa ya meno na jinsi ya kuzuia matatizo ya baadaye.
Chris ni mkarimu sana na mara nyingi hujitolea. Alijitolea katika makazi ya wazee kuwasaidia wakazi ambao hawakuweza kutoka katika makazi hayo ili kupata huduma za kuzuia matatizo ya meno. Pia alifanya safari ya kujitolea kwenda Amerika Kusini ambako alisaidia kujenga majengo mapya kwa watoto wasio na makazi. Chris pia alijitolea nchini Ufilipino alipokuwa katika Jeshi la Wanamaji. Huko alitoa huduma za meno kwa wakazi wa visiwa vya mbali ambako hakukuwa na huduma hizo. Chris anapokuwa na muda wa ziada, anapenda kusafiri na familia yake, kufanya kazi za useremala, kunyanyua uzani na kucheza mchezo wa kuunda timu za kubuni za futiboli ya Marekani. Wakati wa msimu wa futiboli ya Marekani, anapenda kuishangilia timu yake anayoipenda zaidi, Pittsburg Steelers.
Huduma za meno zinazokua pamoja nawe na familia yako katika kliniki kote Missouri. Pia tunakubali Medicaid.

Bila miadi Huduma za Meno Tiba ya Familia Huduma za Afya ya Watoto
Jumatatu–Ijumaa: 07:30 – 17:00 Jumamosi–Jumapili: Imefungwa
Unaweza kupanga miadi na Chris Heinzel kwa kutupigia simu au kuomba miadi kupitia MyChart.